Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu-logo

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

United Nations

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Location:

New Rochelle, NY

Description:

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twitter:

@HabarizaUN

Language:

Swahili

Contact:

9178215291


Episodes
Ask host to enable sharing for playback control

13 MEI 2025

5/13/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika lengo namba moja la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG1 la kutokomeza umaskini na inatupeleka nchini Tanzania ambako Umoja wa Mataifa umeona bora kusaidia wafugaji kuku kuondokana na umaskini.Katika mkutano wa ngazi ya mawaziri kuhusu mustakabali wa ulinzi wa amani unaofanyika leo mjini Berlin Ujerumani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza vipaumbele vitatu vya msingi katika mageuzi ya ulinzi wa amani kwa muktadha wa dunia inayobadilika kwa kasi.Mashariki ya Kati leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limeonya kuhusu vifo vya watoto kutokana na utapiamlo Gaza, sababu kubwa ikiwa ni kuendelea kukosekana kwa msaada wa kibinadamu unaojumuisha lishe maalum kwa watoto.Wakati mahitaji ya kibinadamu yakizidi kuongezeka duniani watu milioni 308 katika nchi 73 wakihitaji msaada wa dharura , Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women limeonya kuwa wanawake na wasichana ndio wanaoathirika zaidi wa migogoro, wakikumbwa na utapiamlo, vifo vinavyoweza kuzuilika vinavyohusiana na ujauzito, na ukatili wa kingono kwa kiwango cha juu, huku mfumo wa misaada ya kibinadamu ukikumbwa na ukata wa fedha.Na katika mashinani, fursa ni yake Jean Todt, Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu usalama barabarani akieleza ni jambo gani lifanyike kuhakikisha usalama barabarani wakati huu dunia inaadhimisha Wiki ya Usalama Barabarani maudhui yakijikita kwenye kuhakikisha barabara ni salama kwa ajili ya waenda kwa miguu na waendesha baiskeli.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Duration:00:11:36

Ask host to enable sharing for playback control

Teknolojia inatatua changamoto za kijamii Wasichana katika TEHAMA

5/12/2025
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA, au ICT inaendelea kutawala na kuunda fursa mpya, lakini wanawake bado wanakumbana na changamoto kubwa ya upungufu wa uwakilishi. Hata hivyo, wanawake wanavuka mipaka na sasa Bi. Joy, msichana kutoka Nairobi Kenya, ambaye ni mtaalamu katika teknolojia ya kidijitali, amekalia nafasi muhimu katika kubadili mtindo wa maisha kupitia elimu ya ICT. Katika mahojiano na washirika wetu Radio Domus, alizungumzia umuhimu wa kuhamasisha wasichana kujiunga na masomo ya teknolojia ili kutengeneza mustakabali mpya wa kidijitali, na kubadili dunia kwa njia ya kidigitali na usawa. Sharon Jebichii na Makala zaidi

Duration:00:03:38

Ask host to enable sharing for playback control

12 MEI 2025

5/12/2025
Hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi vyaliacha hoi bara la Afrika yaonya WMO.WHO yahaha kukabiliana na kipindupindu Angola.Makala Sharon Jebichii anatupeleka nchini Kenya, kumulika masuala ya wasichana katika ICT.Mashinani leo inaangazia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa wiki ya usalama barababarni.

Duration:00:11:43

Ask host to enable sharing for playback control

WHO na vita dhidi ya kipundupindu Angola.

5/12/2025
Tangu Januari mwaka huu 2025 nchini Angola, ugonjwa wa kipindupindu umesambaa katika majimbo 17 kati ya 21 ya nchi hiyo. Mlipuko huu tayari umesababisha karibu vifo 600 linaeleza Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO. António Catunda, ni Msimamizi wa Uhamasishaji wa Afya katika kituo cha afya cha Sambizanga jimboni Luanda unakopatikana mji Mkuu wa Angola. Kupitia video iliyoandaliwa na WHO, anaielezea hali ilivyo.

Duration:00:02:15

Ask host to enable sharing for playback control

Hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi vyaliacha hoi bara la Afrika yaonya WMO.

5/12/2025
Ripoti mpya kuhusu “Hali ya Hewa Afrika 2024” iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO imeonya kwamba muongo wa joto zaidi kuwahi kushuhudiwa Afrika umeleta madhara makubwa kwa bara hilo. Evarist Mapesa na taarifa zaidi

Duration:00:02:12

Ask host to enable sharing for playback control

Chokoleti itengenezwayo Uganda yavuka mpaka na mabara -UNCTAD

5/9/2025
Kutoka kakao ghafi huko Bundibugyo, magharibi mwa Uganda hadi Kampala mji mkuu wa kibiashara wa taifa hilo la Afrika Mashariki ndiko kunapatikana kiwanda cha kutengeneza chokoleti cha Equator kinachomilikiwa na Barbara Gonget na mume wake Gustav. Awali wazo la biashara hii lilionekana kutokuwa na mashiko. Ingawa hivyo baada ya ITC, ambacho ni Kituo cha Kimataifa ha Biashara kilicho chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, UNCTAD pamoja na wadau wao kuweka usaidizi wao, hali imebadilika na sasa biashara inavuka sio tu mipaka bali mabara. Wawili hao Kwa kuchanganya mbinu za hali ya juu, zinazojali jamii, na ufundi wa kitaalamu, wanabadili taswira ya uzalishaji wa chokoleti nchini humo.Je wamefanya nini? Assumpta Massoi anafafanua zaidi kwenye makala hii iliyofanikishwa na ITC.

Duration:00:03:55

Ask host to enable sharing for playback control

Mashirika ya UN yakemea mpango wa Israel kutumia misaada kama mtego - Gaza

5/9/2025
Mpango wa Israel wa kuchukua udhibiti wa misaada ya dharura huko Gaza utaweka maisha ya raia hatarini na kusababisha ufurushwaji Mkubwa wa watu huku ikitumia misaada kama mtego, walisema leo wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa. Anold Kayanda anafafanua zaidi

Duration:00:01:44

Ask host to enable sharing for playback control

09 MEI 2025

5/9/2025
Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Gaza: Mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yakemea mpango wa Israel kutumia misaada kama mtego-Mradi wa HOTIGRO wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini Tanzania wainua wakulima wa mboga na matunda -Makala leo inatupeleka Uganda kumulika kiwanda cha kutengeneza chokoleti-Na mashinani tunabisha hodi Kenya kunakofanyika mkutano wa UNESCO kuhusu urithi wa utamaduni wa Afrika

Duration:00:09:57

Ask host to enable sharing for playback control

Kutimiza azimio la watu wa jamii za asili ni jukumu la mataifa yote kote duniani - Adam Kulet Ole Mwarabu

5/8/2025
Jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa jamii za asili limekunja jamvi mwishoni mwa wiki iliyopita hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na kandoni mwa jukwaa hilo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro nchini Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu, wamejadili mengi lakini Ole Mwarabu anaanza kwa kukumbusha alichokibeba kwenye jukwaa la mwaka jana kinavyotekelezwa nchini mwake.

Duration:00:06:48

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "DALALI”

5/8/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DALALI”
Ask host to enable sharing for playback control

08 MEI 2025

5/8/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa ambayo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro nchini Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu.Wiki kumi baada ya kuanza kwa mzingiro kamili wa Israel dhidi ya wakazi wa Gaza, zaidi ya robo tatu ya kaya katika eneo la Palestina kuna uhaba mkubwa wa huduma ya maji, huku hali ya usafi ikizidi kuwa mbaya, yameonya leo mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu athari za "uhaba huo wa maji kwa kuzingatia kuwa msimu wa joto unakaribia.”Ripoti kutoka Sudan zikidai kwamba juzi jumatano kulikuwa na jaribio la mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani dhidi ya kitovu muhimu cha misaada nchini humo juzi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia tamko alilolitoa jana jioni kwa saa za New York, Marekani, ameongeza nguvu yake katika kutoa wito unaozidi kuwa wa muhimu kuhamasisha kuanzishwa kwa mazungumzo ya amani ya kweli.Kufuatia kuendelea kwa mvutano wa majirani, India na Pakistani, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Philemon Yang, ametoa wito wa kuzitaka nchi hizo mbili kuchukua tahadhari na kuepuka hatua zinazoweza kuongeza mzozo. Balozi Yang anasisitiza mazungumzo ya amani na kufuata sheria za kimataifa ndiyo njia pekee ya kusuluhisha migogoro.”Na katika jifunze Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "DALALI”Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:11:12

Ask host to enable sharing for playback control

Operesheni za kijeshi Jammu na Kashmir hazina tija – Guterres

5/7/2025
Huko barani Asia majirani wawili India na Pakistani wameendelea kuoneshana mvutano kati yao kwenye eneo la Jammu na Kashmiri tangu tarehe 22 mwezi uliopita wa Aprili baada ya shambulizi huko Pahalgam. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kama anavyoelezea Assumpta Massoi.

Duration:00:02:07

Ask host to enable sharing for playback control

07 MEI 2025

5/7/2025
Hii leo jaridani tunaangazia mvutano unaoendelea barani Asia kati ya majirani wawili India na Pakistani, na msaada wa mguu bandia uliowezesha mtototo nchini Kenya kwenda shule. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunakwenda katika ukanda wa Gaza.Huko barani Asia majirani wawili India na Pakistani wameendelea kuoneshana mvutano kati yao kwenye eneo la Jammu na Kashmiri tangu tarehe 22 mwezi uliopita wa Aprili baada ya shambulizi huko Pahalgam. Katibu Mkuu ametoa wito kwa mara nyingine tena.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau wameleta neema kwa watoto wanaoishi na ulemavu katika Kaunti ya Kisumu Magharibi mwa Kenya baada ya kuwapa msaada wa vifaa ikiwemo viti mwendo na viungo bandia kupitia mradi wa ubunifu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, msaada uliobadili maisha yao.Makala katika wiki ya chanjo duniani, iliyotamatishwa tarehe 30 wiki iliyopita, mtaa wa Butiama, ulioko Mtoni Kijichi katika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania ulishuhudia wazazi na walezi wakijitokeza kuwapatia watoto wao chanjo muhimu za kuwalinda dhidi ya maradhi hatari. Miongoni mwao ni Hija Halfani ambaye alimpeleka mtoto wake mwenye umri wa siku 42 kupata chanjo yake ya kwanza.”Na mashinani mashinani, kama sehemu ya juhudi za kutoa nafasi ya kujieleza kisanii na kuwaunga mkono Wapalestina kihisia (emotional support), UNRWA imeandaa maonesho ya sanaa katika Shule ya Al-Rimal, ambayo sasa ni makazi ya wakimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza, na watoto walipata fursa ya kuonesha kazi za sanaa zinazoakisi(reflect) madhila wanayopitia wakati wa vita kati ya Israeli na Hamas ambavyo bado vinaendelea. Malak Fayad, msichana mkimbizi kutoka Beit Hanoun ni mmoja wao akionesha sanaa yake.….Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:10:54

Ask host to enable sharing for playback control

Wazazi pelekeni watoto wenu kupata chanjo dhidi ya maradhi - Bi. Halfani

5/7/2025
Katika Wiki ya Chanjo duniani, iliyotamatishwa tarehe 30 wiki iliyopita, mtaa wa Butiama, ulioko Mtoni Kijichi katika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania ulishuhudia wazazi na walezi wakijitokeza kuwapatia watoto wao chanjo muhimu za kuwalinda dhidi ya maradhi hatari. Miongoni mwao ni Hija Halfani ambaye alimpeleka mtoto wake mwenye umri wa siku 42 kupata chanjo yake ya kwanza. Je, ni mafanikio gani yamepatikana na kwa nini chanjo hizi ni muhimu? Ungana na Sharon Jebichii kwa makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania.

Duration:00:03:36

Ask host to enable sharing for playback control

Evelyn Atieno: Asante UNICEF kwa kubadili Maisha ya mwanangu Fidel

5/7/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau wameleta neema kwa watoto wanaoishi na ulemavu katika Kaunti ya Kisumu Magharibi mwa Kenya baada ya kuwapa msaada wa vifaa ikiwemo viti mwendo na viungo bandia kupitia mradi wa ubunifu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, msaada uliobadili maisha yao. Flora Nducha amefuatilia tabasamu la mama ambaye mwanye amenufaika na kiungo bandia ungana naye kwa tarifa zaidi

Duration:00:02:32

Ask host to enable sharing for playback control

06 MEI 2025

5/6/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa makao makuu ambako Idhaa hii Dokta Willis Ochieng kutoka Kenya aliyehudhuria ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kilimo na maendeleo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na mashinani tunakwenda Ghana.Ukuaji wa maendeleo ya binadamu – yanayopimwa kwa uhuru na ustawi wa watu – umeendelea kuwa wa kasi ndogo tangu mshtuko mkubwa wa janga la COVID-19 lakini kuna matumaini makubwa kwamba Akili Mnemba au AI, ikiwa itatumika kwa njia sahihi, inaweza kuwa chombo chenye nguvu cha kuboresha maisha ya mamilioni ya watu. Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya kila mwaka ya Maendeleo ya Binadamu iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP.Kulengwa kwa hospitali ya Médecins Sans Frontières nchini Sudan Kusini kunaweza kuwa uhalifu wa kivita imeeleza leo Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Sudan Kusini kufuatia mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa dhidi ya hospitali ya Médecins Sans Frontières (MSF) huko Old Fangak, Jimbo la Jonglei mapema majuzi asubuhi ya Jumamosi na kusababisha vifo vya takribani raia saba na kujeruhi wengine. Shambulio hilo lilifanyika baada ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) kutoa onyo la kufanya shambulizi iwapo dai lao la kuachiliwa meli zao zilizotekwa halitatekelezwa.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, iliyotolewa leo imeonesha jinsi mahali mtu anakozaliwa kulivyo na mchango katika maisha yake. Ripoti inasema, “mahali mtu anakozaliwa huweza kuamua kama ataishi zaidi ya miongo mitatu kuliko mtu mwingine aliyezaliwa katika nchi yenye hali duni za makazi, elimu na fursa za ajira.”Na mashinani leo nampa fursa Dorcas Awortwe, Naibu Mkurugenzi wa Tume ya Maendeleo ya Kanda ya Kati kutoka Ghana, aliyeshiriki kwenye mkutano wa jukwaa la watu wa asili hapa Makao Makuu wiki iliyopita anazungumzia changamoto zinazowakabili watu wa asili katika jamii yake na ombi lake kwa Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:12:03

Ask host to enable sharing for playback control

VoTAN sio tu mtandao wa kidijitali kusaidia manusura wa ugaidi bali pia ni familia - Manusura

5/5/2025
Hatimaye kilio cha manusura wa ugaidi duniani cha kuwa na Mtandao wa Mashirika yao ili kuweza kupaza zaidi sauti zao kwa ajili ya sio tu kusaidiwa bali pia kuepusha matukio kama hayo, kimepata jawabu baada ya Mtandao huo au VoTAN kuzinduliwa kwenye Umoja wa Mataifa. Kwa msaada wa kifedha kutoka Hispania, Iraq na nchi nyingine wanachama, mtandao huu ulio chini ya Programu ya kusaidia manusura wa ugaidi kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kukabilana na Ugaidi, UNOCT, unatarajiwa kuziba mapengo ya msaada na kuinua ushuhuda wa manusuta kutoka maeneo yaliyopuuzwa duniani. Assumpta Massoi amefuatilia uzinduzi huo na kuandaa makala hii.

Duration:00:05:02

Ask host to enable sharing for playback control

MONUSCO yapatia wanawake wakimbizi DRC mafunzo ya ushoni

5/5/2025
Wanawake 125 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kigonze, karibu na Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ghasia huripokiwa mara kwa mara, sasa wana matumaini mapya ya kujikwamua kiuchumi baada ya kujiunga na mradi wa mafunzo ya kushona nguo unaofadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO). Sharon Jebichii na taarifa kamili.

Duration:00:02:31

Ask host to enable sharing for playback control

05 MEI 2025

5/5/2025
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya wakunga na kazi zao muhumi, na mafunzo ya jerahani kwa wakimbizi wa ndani nchini DRC. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakwenda Gaza.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wakunga, tunakwenda nchini Tanzania kummulika mkunga ambaye alinusuru maisha ya wajawazito wawili wakati wa mafuriko makubwa ya Novemba 2023 wilayani Hanang, mkoani Manyara, kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ikiwa ni ushuhuda wa majukumu mazito yanayokumba wakunga.Wanawake 125 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kigonze, karibu na Bunia, mji mkuu wa jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ghasia huripokiwa mara kwa mara, sasa wana matumaini mapya ya kujikwamua kiuchumi baada ya kujiunga na mradi wa mafunzo ya kushona nguo unaofadhiliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo (MONUSCO).Makala Assumpta Massoi anamulika uzinduzi wa mtandao wa Mashirika ya Manusura wa Ugaidi duniani, VoTAN uliofanyika wiki iliyopita hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Na mashinani kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), fursa ni yake Rawhiyeh, mkimbizi kutoka Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israel ambaye anasimulia kwa uchungu madhila yanayowakumba yeye na familia yake baada ya kupoteza makazi yao kutokana na mashambulizi ya mabomu.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:10:56

Ask host to enable sharing for playback control

Mkunga nchini Tanzania atoa wito wa uwekezaji kwenye fani hiyo

5/5/2025
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wakunga, tunakwenda nchini Tanzania kummulika mkunga ambaye alinusuru maisha ya wajawazito wawili wakati wa mafuriko makubwa ya Novemba 2023 wilayani Hanang, mkoani Manyara, kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ikiwa ni ushuhuda wa majukumu mazito yanayokumba wakunga. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Duration:00:02:07